Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Rais wa Ivory Coast Alassane Outtara anatarajiwa kurejea madarakani katika uchaguzi mkuu nchini humo unaofanyika hii leo, miaka mitano baada ya uchaguzi uliopita kukumbwa na ghasia. Outtara alimshinda Laurent Gbagbo mwaka 2010 lakini Gbagbo alikataa kuachia madaraka na kuchochea ghasia zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya 3,000 na maelfu kuachwa bila ya makaazi. Outtara anatumai kushinda uchaguzi huo wa leo kwa kishindo kutokana na kazi yake nzuri ya kuuimarisha uchumi wa taifa hilo, miundo mbinu na kuimarisha pia usalama. Wagombea watatu wa upinzani kati ya kumi wamejiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho wakidai zoezi hilo la upigaji kura limekumbwa na dosari. Watu milioni sita wamesajiliwa kupiga kura.
Mwisho wa habari/ 291